1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Familia ya kifalme yaadhimisha miaka 10 ya kifo cha Princess Diana

31 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUA

Famila ya malkia nchini Uingereza inaadhimisha miaka kumi tangu kufa kwa Princess Diana kufuatia ajali ya barabarani nchini Ufaransa.

Marehemu Princess Diana atapongezwa katika ibada ya ukumbusho itakayongozwa na Askofu wa Canterbury aliye pia kiongozi wa kanisa la Kianglikana nchini Uingereza .

Diana alifariki Agosti 31 akiwa na umri wa miaka 36 pale gari aina ya Liomousine alimokuwa akisafiri pamoja na mepnzi wake Dodi al Fayed lilipopata ajali kwenye njia ya chini kwa chini mjini Paris,Ufaransa.

Wakazi katika eneo la nyumba yake ya zamani la Kensington Palace waliweka mashada ya maua ili kutoa heshima zao za ukumbusho.Ibada hiyo ya ukumbusho inafanyika katika kanisa la Kijeshi la Wellington Barracks.

Zaidi ya jamaa 30 wa familia ya kifalme waanahudhuria ibada hiyo akiwemo muwe wake wa zamani Prince Charles,wanawe William na Harry waliokuwa na umri wa miaka 15 na 12 wakati wa kifo cha mama yao.Waziri Mkuu Gordon Brown na wa zamani Tony Blair ni baaadhi ya wageni 500 walioalikwa kwenye ibada hiyo.

Hata hivyoBi Camilla aliye Duchess wa Cornwall na mkewe Prince Charles hatahudhuria ibada hiyo kwa sababu binafsi japo alialikwa na watoto wa mume wake.Mohamed al Fayed babake mpenzi wake marehemu Princess Diana Dodi al Fayed hatahudhuria ibada hiyo kwani hakualikwa.Bwana al Fayed ni mfanyibishara mkubwa mjini London na mwenye duka la bidhaa ghali maarufu la Harrods.

Uchunguzi rasmi mwengine unaanza Octoba tarehe 2 ili kugundua chanzo cha kifo chake.