1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Wanamaji watishiwa kisaikolojia

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBt

Wanamaji 15 wa Uingereza wamekuwa na mkutano na waandishi wa habari katika kambi ya kijeshi nchini Uingereza ambapo wamesema walivuliwa nguo na kuzibwa macho pamoja na kutiwa pingu kama sehemu ya vitisho vya kisaikolojia wakati walipokuwa wakishikiliwa nchini Iran.

Wanajamaji hao wamesisitiza kwamba walikuwa kwenye eneo la bahari ya Iraq wakiendesha operesheni zao za kawaida wakati walipozingirwa na wanajeshi wa Iraq na kutekwa na kwamba kupambana nao halikuwa chaguo muafaka wakati huo.

Wamesema wakati walipowasili nchini Iran walitenganishwa na kukatiwa moja kwa moja mawasiliano na mtu yoyote yule ambapo walikuwa wakishinikizwa kisaikolojia mfululizo.

Wanamaji hao wakiwa wamezibwa macho waliwekwa dhidi ya ukuta wakati walinzi wa Iran wakitayarisha silaha zao tayari kama vile kwa ajili ya kuzifyatuwa.Waliambiwa kwamba iwapo hawatokiri kufanya makosa ya kuingia kwenye eneo la bahari ya Iran watakabiliwa na vifungo vya miaka saba gerezani.

Iran imeuelezea mkutano huo na waandishi wa habari kuwa propaganda.