1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Wanamaji 15 wa Uingereza warudi nyumbani

6 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCC8

Wanamaji 15 wa Uingereza wamerudi nyumbani baada ya kushikiliwa kwa takriban wiki mbili nchini Iran.

Wanajeshi hao ambao ni wanaume 14 na mwanamke mmoja wamerudi London kwa kutumia ndege ya abiria ya shirika la ndege la Uingereza British Airways hapo jana.Baadae walipelekwa katika kambi ya kijeshi kusini magharibi mwa Uingereza ambapo walihojiwa na kuarifiwa.

Akizungumza nje ya ofisi yake mjini London Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amekaribisha kuachiliwa kwao ambapo amesema kumefanyika bila ya masharti licha ya kwamba serikali ya Iran imedai kwamba Uingereza imeomba radhi kwa maandishi kwa kuingia kwenye eneo la bahari ya Iran.

Wanamaji hao 15 wa Uingereza walitekwa na wanajeshi wa Iran kwa kile serikali ya Iran ilichosema kwamba katika bahari yake kwenye Mlango Bahari wa Shatt al Arab wakati Uingerezea ikiendelea kusisitiza kwamba walikuwa kwenye eneo la bahari ya Iraq wakati huo.