1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON :Wanaharakati waandamana katika mataifa 30 kwa ajili ya Darfur

17 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBP8

Waandamanaji wamefanya maandamano katika mataifa kadhaa kutoa wito kwa viongozi wa ulimwengu na Baraza la Umoja wa Matifa kutia juhudi zaidi kumaliza tatizo la Darfur nchini Sudan.Waandamanaji mjini Roma nchini Italia walivaa tshirt nyeupe zilizokuwa na picha ya mkono uliolowa damu na kuelekea katikati ya mji.Kulingana na waandalizi wa maandamano hayo yaliyofanyika kwenye zaidi ya mataifa 30 yakiwemo Australia,Misri,Ujerumani,Japan,Mongolia,Nigeria,Afrika kusini na Marekani---jamii ya kimataifa imepunguza kasi yake tangu Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuidhinisha kupelekwa kwa kikosi cha majeshi alfu 26 kilichoimarishwa cha Umoja wa mataifa na Afrika kulinda amani Darfur. Mjini London waandamanaji hao waliandamana kwenye ubalozi wa Sudan ulio karibu na afisi za Waziri Mkuu Gordon Brown.

''Kama hakuna kitakachofanyika na ahadi zote hazitatimizwa nadhani tutalazimika kuwa wazi kuwa endapo serikali ya Sudan haifanyi mabadiliko yanayohitajika tutaiwekea vikwazo zaidi.Naamini Marekani na mataifa ya ulaya yataunga mkono hoja hiyo''