1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Wairaki milioni nane wanahitaji msaada kwa haraka

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdm

Wairaki takriban milioni nane wanahitaji msaada wa dharura huku watoto wakiwa wameathiriwa zaidi na hali inayoendelea kuwa mbaya.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo mjini London Uingereza na shirika la Oxfam na muungano wa mamshirika yasiyo ya kiserikali nchini Irak.

Idadi hiyo inajumulisha watu milioni mbili wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na wanahitaji kwa haraka misaada mbalimbali ya kiutu.

Ripoti hiyo imesema Wairaki milioni mbili wamelazimika kuyahama makazi yao nchini mwao na milioni mbili wengine ni wakimbizi.

Wakimbizi wengi wamekimbilia nchi jirani za Jordan na Syria katika mzozo ambao ripoti hiyo imeuleza kuwa mbaya zaidi wa wakimbizi duniani. Wimbi la wakimbizi nchini Jordan na Syria limesababisha matatizo makubwa katika utoaji wa huduma za afya, elimu na huduma za kijamii.

Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa limeitaka jumuiya ya kimataifa izisaidie kifedha Syria na Jordan kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi wa Irak.