1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Waingereza wanataka majeshi ya nchi yao yalioko Irak yarudishwe nyumbani

24 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzh

Idadi kubwa ya raia wa Uingereza wanataka majeshi ya nchi yao yalioko Irak yarejeshwe nyumbani. Hayo ni kulingana na kura mbili za maoni. Kura ya kwanza ya maoni ambayo ilifanywa na taasisi ya utafiti, ICM, inasema asili mia 60 ya watu wanataka majeshi ya Uingereza yalioko Irak yarudishwe nyumbani kabla ya mwaka huu kumalizika. Asili mia 45 wangependelea hilo lifanyike sasa hivi wakati asili mia 16 wakikubali kusubiri mpaka mwishoni mwa mwaka huu.

Kura nyingine ya maoni iliochapishwa katika gazeti la ´´Independant´´, imeonesha kuwa asili mia 62 wangependa majeshi hayo yarudishwe nyumbani haraka iwezekanavyo.

Ni asili mia 30 tu ya watu ambao wangependelea wanajeshi wa Uingereza wabaki nchini Irak kwa muda wote unaohitajika wao kuweko katika nchi hiyo.

Uingereza iliwatuma wanajeshi 7,200 nchini Irak, wengi wao wakiwa katika eneo la kusini mwa nchi.