1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uchunguzi wa mwili wa Litvinenko kufanyika leo.

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnn

Uchunguzi wa mwili wa jasusi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko utafanyika leo wakati watu zaidi wanachunguzwa kuhusiana na miale ya sumu.

Kiasi kikubwa cha miale ya Polonium 210 ilipatikana katika mkojo wa Litvinenko.

Ndege nne za shirika la ndege la British Airways pia zimechunguzwa iwapo zina miale hiyo.

Shirika hilo linataka kuwachunguza wasafiri 33,000 na wafanyakazi 3,000 iwapo wameathirika na miale hiyo.

Wakati huo huo msemaji wa waziri mkuu wa zamani wa Urusi msemaji wa waziri mkuu wa zamani wa Urusi Yegor Gaidar amesema kuwa alikuwa mhanga wa tukio lisilokuwa la kawaida la kupewa sumu.

Polisi nchini Ireland, ambako Gaidar alikuwa mgonjwa, wameanza uchunguzi kuhusiana na sababu za ugonjwa wake.