1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Scotland Yard yachunguza iwapo chama tawala kilipewa hongo.

15 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjK

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amehojiwa na polisi , wanaochunguza iwapo chama tawala cha Labour kimetoa upendeleo wa serikali ili kujipatia fedha. Msemaji wa waziri mkuu amesema kuwa Blair alihojiwa kama shahidi na sio kama mtuhumiwa. Kiasi watu 90 wamehojiwa hadi sasa. Uchunguzi huo ulianza baada ya kugundulika kuwa chama cha Labour kimepewa mikopo ya siri kabla ya uchaguzi wa mwaka jana. Baadhi ya wafadhili baadaye waliteuliwa kupata tuzo za heshima. Kitengo cha Scotland Yard kimeashiria kuwa kinatarajia kutoa taarifa ya uchunguzi wao mwezi ujao.