1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Polisi wanaendelea kuwahoji washukiwa

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVv

Nchini Uingereza,polisi wamepewa muda zaidi kuwahoji washukiwa 9 waliokamatwa kuhusika na madai ya kufanya njama ya kutaka kumteka nyara na kumkata kichwa mwanajeshi wa Kiislamu anaetumikia jeshi la Uingereza.Washukiwa 3 walifikishwa mbele ya jaji,siku moja baada ya kukamtwa mjini Birmingham.Polisi wamepewa siku saba zaidi kuwahoji watu hao watatu na wengine 6 walioamua kubakia katika kituo cha polisi.Kuambatana na sheria za Uingereza kupiga vita ugaidi,washukiwa hao wanaweza kuzuiliwa hadi siku 28 bila ya kushtakiwa.