LONDON : Ndege kuzuiliwa kuruka Dafur | Habari za Ulimwengu | DW | 14.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Ndege kuzuiliwa kuruka Dafur

Marekani na Uingereza zinafikiria kupiga marufuku kuruka kwa ndege kwenye anga la eneo la Dafur magharibi mwa Sudan iwapo serikali ya nchi hiyo itatendelea kupinga uwekaji wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair alilizusha suala hilo wakati wa mkutano wake wiki iliopita na Rais George W. Bush wa Marekani.Hatua hiyo inakusudia kuzuwiya matumizi ya ndege za serikali ya Sudan kuunga mkono mashambulizi kwa vijjiji vya Dafur.

Wakati huo huo Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa limekubali kutuma ujumbe wake kwenye eneo hilo la vurugu.Baraza hilo limesema ujumbe wake huo utajaribu kufanya uchunguzi juu ya madai ya kuendelea kwa mateso dhidi ya raia hali ambayo inaelezewa kuwa inazidi kuwa mbaya.

Mzozo uliodumu kwa miaka mitatu huko Dafur kati ya serikali na waasi umesababisha vifo vya watu 200,000 na kuwapotezea makaazi wengine milioni mbili na nusu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com