1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON :Mwanawe Idi Amin ahukumiwa kifungo cha miaka 5

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcT

Mwanawe wa kiume Rais wa zamani wa Uganda marehemu Idi Amin amefungwa jela kwa miaka mitano baada ya kuhusika na genge moja lililosababisha kifo cha mtu mmoja.Kwa mujibu wa Idara ya mashtaka nchini Uingereza Faisal Wangita aliye na umri wa miaka 25 alihusika na kundi la watu 40 waliomshambulia kijana mmoja wa Kisomali Mahir Osman wa miaka 18 mjini London mwanzoni mwa mwaka jana.

Osman alichomwa kisu mara 20 kupingwa mateke na ngumi jambo lililosababisha kifo chake baada ya dakika moja.Tukio hilo lilinaswa na kamera.Watu 13 walishtakiwa katika kesi hiyo iliyokamilika mwezi Aprili na wengine 3 kupatikana na kosa la kusababisha mauaji.Wangita alisamehewa shtaka la kifo mwezi Aprili lakini kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kuhusika na njama hiyo.

Kwa mujibu wa hati rasmi Wangita alizaliwa nchini Uganda ila alielezea polisi kuwa alizaliwa Saudia.Majaji walioendesha kesi hiyo hawakuarifiwa kuwa Wangita alikuwa mwanawe marehemu rais Idi Amin kwani ilidhaniwa kuwa jambo hilo lingeathiri matokeo.