1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina upatiwe suluhu

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsw

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amezihimiza Syria na Iran zijitolee zaidi kusuluhisha mgogoro wa Mashariki ya Kati,hatua ambayo huenda hata ikasaidia kuleta amani nchini Irak.Katika hotuba yenye ujumbe maalum,Blair amesema mgogoro wa Irak unapaswa kutazamwa kama sehemu ya kile alichokiita "Mkakati mzima wa Mashariki ya Kati". Akaongezea kuwa mkakati huo uanze kwa kuutenzua mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina.Kuhusu ushirikiano wa kimataifa,Blair amesema ni muhimu kudumisha ushirikiano imara wa Uingereza pamoja na Marekani na Umoja wa Ulaya.