1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Mabaharia wakatazwa kuuza habari

10 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAw

Waziri wa ulinzi wa Uingereza, Des Brown, amewakataza mabaharia wote 15 waliozuiliwa na Iran kwa siku 13 wasiuze tena habari kwa vyombo vya habari.

Waziri Brown amechukua uamuzi huo baada ya wizara yake kushutumiwa kwa kuwaruhusu mabaharia hao kupokea malipo kwa mahojiano waliyofanya na vyombo vya habari nchini Uingereza.

Mzozo ulianza mwishoni mwa juma lililopita wakati mwanamke pekee miongoni mwa wanamaji hao, Fay Turney, alipozungumza na vyombo vya habari vya Uingereza kueleza kwa kina yaliyomfika wakati alipokuwa akizuiliwa mjini Tehran. Alisema waliomhoji walimtisha kumuua.

Iran ilionyesha picha za mabaharia wa Uingereza wakicheza mchezo wa tennis na kutazama mechi ya ligi ya Uingereza kwenye runinga.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Des Brown amesema sheria zitachunguzwa upya kuhusu malipo kwa ajili ya habari zinazouzwa kwa vyombo vya habari. Wengi wamewakosoa mabaharia wote 15 kwa kunufaika kutokana na kuzuiliwa kwao nchini Iran.

Sambamba na taarifa hizo, Uingereza imetangaza kamba jeshi lake la maji litaanza tena shuhguli za kuchunguza vyombo vya usafiri katika bahari ya ghuba la Uajemi. Kazi hiyo ilisitishwa kufuatia kukamatwa kwa mabaharia 15 wa Uingereza na jeshi la mapinduzi la Iran.