1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Kitisho cha mafuriko kaskazini mwa Ulaya

9 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C78t

Kimbunga kikakli kinatazamiwa kuvuma katika pwani ya Bahari ya Kaskazini ikihofiwa kitasababisha mafuriko mabaya kabisa tangu miaka 20 iliyopita. Mitambo ya kuchimbia mafuta baharini,nje ya pwani ya Norway imefungwa.Hata nchini Uholanzi,bandari ya Rotterdam ambayo ni kubwa kabisa barani Ulaya imefungwa.Ujerumani pia,katika mwambao wa Bahari ya Kaskazini kumetolewa onyo la mafuriko.