1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Kifo cha Diana sio njama ya mauaji

Uchunguzi wa polisi nchini Uingereza umebaini kwamba Princess Diana alikuwa sio muhanga wa njama ya mauaji.

Princess huyo wa Wales alikufa katika ajali ya gari mjini Paris hapo mwaka 1997 akiwa pamoja na mpenzi wake Dodi al Fayed na dereva wake.Mpelelezi mkuu John Stevens amesema uchunguzi huo wa polisi wa miaka 3 umegunduwa kwamba madai ya mauaji kwa kifo cha Diana na Dodi kuwa hayana msingi.Pia amesema kwamba wapenzi hao wawili walikuwa hawakufunga uchumba wakati wa vifo vyao na kwamba Diana alikuwa sio mjamzito.

Uchunguzi huo unakusudia kumaliza karibu muongo mzima wa tuhuma kwamba kifo cha Princess Daina kimetokana na njama za mauaji.

Hata hivyo baba wa Dodi ametupilia mbali matokeo ya uchunguzi ya repoti hiyo kuwa ni takataka tu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com