1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Bunge laidhinisha silaha za kinuklia kufanyiwa ukarabati.

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIx

Bunge la Uingereza limepiga kuwa kuunga mkono kuzifanya za kisasa silaha za kinuklia katika nyambizi za nchi hiyo.

Baada ya mjadala wa saa sita , wabunge 409 walipiga kura kwa ajili ya mpango huo na 161 walipinga.

Lakini hoja hiyo ilipitishwa kutokana na kuungwa mkono na chama cha kihafidhina kilichoko katika upinzani, baada ya wabunge kadha wa chama tawala cha Labour kupiga kura dhidi ya serikali yao.

Akizungumza kabla ya kupiga kura , waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema kubadilishwa kwa mfumo wa makombora ya kinuklia ni muhimu kwa ajili ya usalama wa nchi hiyo.

Wapinzani wa hoja hiyo wanasema kuwa Waingereza wengi wanapinga kuboresha makombora hayo na wanadai kuwa hatua hiyo inaweza kuathiri juhudi za kuizuwia Iran kujipatia silaha za kinuklia pamoja na nchi nyingine.