1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Brown kupunguza wanajeshi Iraq.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HC

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema kuwa serikali yake itapunguza idadi ya wanajeshi wake nchini Iraq kwa zaidi ya nusu, na kufikia wanajeshi 2,500 ifikapo majira ya machipuko mwakani. Waziri mkuu amesema hayo katika hotuba aliyoitoa katika baraza la wawakilishi.

Hii inakuja wiki moja baada ya kuahidi kupunguza idadi ya wanajeshi wa Uingereza nchini Iraq hadi wanajeshi 4,500 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Brown ameliambia bunge kuwa maamuzi yote ya mwisho kuhusiana na kuwaondoa wanajeshi yatafanywa kwa mashauriano na uongozi wa jeshi la Uingereza nchini Iraq.