1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Blair kutangaza siku ya kujiuzulu

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5c

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema kwamba atatangaza juma lijalo lini atakapojiuzulu kutoka kwa wadhifa wake.

Blair ameyasema hayo leo asubuhi wakati wa mahojiano na runinga moja mjini London, miaka kumi tangu chama cha Labour kiliposhinda uchaguzi mkuu na kuingia madarakani nchini Uingereza.

Waziri mkuu Blair amemsifu mrithi wake waziri wa fedha, Gordon Brown, akisema atakuwa kiongozi mahiri.

Sambamba na ripoti hiyo, jopo la wabunge watano wa Uingereza litachunguza jinsi shirika la ujasusi la MI5 lilivyoshughulikia habari kuwahusu washukiwa wawili wa mashambulio ya Julai saba mwaka wa 2005, kufuatia uamuzi wa jana wa mahakama.

Waingereza watano walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kupanga kufanya mashambulio ya mabomu nchini Uingereza mnamo mwaka wa 2004.

Imefichuka kwamba shirika la ujasusi la MI5 lilikuwa likiwachunguza washukiwa wawili wa mashambulio ya Julai saba lakini likashindwa kuwachukulia hatua.