LONDON: Blair ataka wanamaji waachiliwe bila masharti | Habari za Ulimwengu | DW | 30.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Blair ataka wanamaji waachiliwe bila masharti

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameonya juu ya hatua zinazochukuliwa kuifanya Iran iwachilie huru wanajeshi 15 wa Uingereza inayowazuilia. Blair anataka wanajeshi wote waachiliwe bila masharti.

´Hii sio hali inayoweza kutanzuliwa na kitu kingine mbali na kuachiliwa huru bila masharti kwa watu wetu wote.´

Kiongozi wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, amesema umoja huo unakiona kitendo cha Iran kuwa kisicho na uhalali wowote.

Katika barua ya pili inayosemekana iliandikwa na mwanajeshi wa kike aliye miongoni mwa wanajeshi wanaozuiliwa, na iliyotumwa kwa mbunge wake nchini Uingereza,mwanajeshi huyo anasema wanajeshi wa Uingereza walio nchini Irak wanatakiwa waondoke.

Katika barua yake ya kwanza mwanajeshi huyo alikiri kwamba yeye pamoja na wanajeshi wenzake waliingia katika himaya ya Iran.

Jeshi la Uingereza limetoa ramani linazosema zinadhihirisha kwamba wanajeshi wote 15 walikuwa katika eneo la Irak wakati walipokamatwa.

Sambamba na ripoti hiyo rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad ameitaka Uingereza iiombe msamaha Iran kwa wanajeshi wake kuingia katika himaya ya Iran kwenye ghuba ya Uajemi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com