1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Benki ya Barclays kununuwa ABN Amro

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7i

Benki ya Barclays ya Uingereza imefikia makubaliano ya kuinunuwa benki mpizani wake ya Uholanzi ya ABN Amro makubaliano ambayo yataanzisha mojawapo ya benki kubwa kabisa duniani.

Makubaliano hayo yana thamani ya zaidi ya euro bilioni 67. Barclays inasema kwamba takriban ajira 13,000 zinaweza kupunguzwa katika wafanyakazi wake watakaochanganywa pamoja.

Hata hivyo kununuliwa kwa benki hiyo kunaweza kukabiliwa na changamoto kutoka kwa ushirika wa mabenki matatu ya Royal Bank ya Scotland,Santander ya Uhispania na kundi la benki ya Uholanzi na Ubelgiji ya Fortis.