1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lome:Tume ya uchaguzi Togo yajizuwia kutangaza matokeo kamili

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dp

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Togo, imesema leo inachelewesha kutangaza matokeo kamili ya uchaguzi wa bunge uliofanyika wiki iliopita, kwa sababu ya kile kinachoonekana kukiukwa kwa taratibu wakati wa kuhesabiwa kura. Tume hiyo imesema katika taarifa yaker kwa njia ya redio ya taifa kwamba baadhi ya masanduku yaliwasilishwa ofisi ya tume bila ya kufungwa kama inavyotakiwa na kwamba kuna matokeo yaliopatikana kutoka vituo vya uchaguzi ambayo hayamo katika orodha rasmi ya matokeo.