1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LOME : Idadi kubwa yajitokeza uchaguzi wa bunge

15 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fl

Imeripotiwa kwamba idadi kubwa ya wapiga kura imejitokeza katika uchaguzi wa bunge nchini Togo hapo jana.

Chama tawala cha RTP kinapambana na kile cha upinzani cha UFC kwa mara ya kwanza kabisa takriban kwa miongo miwili wakati kiliposusia chaguzi zote zilizopita.Vyama vyote vikuu vya upinzani vilisusia uchaguzi wa mwaka 2003 kutokana na ukosefu wa uwazi na maadalizi mabaya ya uchaguzi huo.

Uchaguzi huu unaonekana kuwa mtihani ambao yumkini ukaamuwa iwapo Umoja wa Ulaya uanze tena kutowa msaada kwa taifa hilo la Afrika magharibi kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 15.