1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Loew amrejesha Boateng kikosini-Wagner badala ya Gomez

Sekione Kitojo
29 Septemba 2017

Timu  ya  taifa  ya  Ujerumani  katika michezo miwili  ya  kufuzu kucheza katika  fainali  za kombe  la  dunia nchini Urusi  mwakani itakuwa  na  mlinzi Jerome Boateng.

https://p.dw.com/p/2kxIZ
Deutschland Trainer Joachim Loew
Picha: picture-alliance/GES/M. I. Guengoer

Mchezaji  huyo  ambaye  alikuwa  katika  kikosi kilichotwaa  kombe  la  dunia mwaka 2014 nchini  Brazil  kutoka  Klabu  ya  Bayern ameitwa katika  kikosi  cha  kocha  Joachim Loew ambapo Oktoba 5 kitapambana  na  Ireland ya  kaskazini  na  siku  tatu  baadaye  mjini Kaiserslautern  kitapambana  na  Azerbaijan.

Symbolbild Jerome Boateng
Jerome Boateng mlinzi wa timu ya taifa na Bayern MunichPicha: picture-alliance/dpa

Kwa upande  wa  ushambuliaji  Sandro Wagner  wa  Hoffenheim  atachukua  nafasi  ya Mario Gomez  wa  Wolfsburg  ambaye  ni  majeruhi, na  pia Timo Werner  ameitwa  kikosini. Pamoja  na  nahodha  Manuel Neuer anakosekana  pia  katika  kikosi  hicho Sami Khedira na  Mesut Ozil.

Ujerumani  inaongoza  kundi C ikipata  ushindi  mara  nane kutokana  na  michezo  minane, kwa  ajili  ya  kufuzu  kucheza  katika  fainali  za  kombe  la  dunia mwaka 2018  nchini  Urusi na  hivi  sasa  inahitaji  pointi  moja  tu katika  mchezo  wa  Alhamis  mjini  Belfast  dhidi  ya Ireland  ya  kaskazini  kuweza kufuzu.

Ireland  inafahamu  kwamba  inaupungufu  wa  pointi  tano nyuma  ya  Ujerumani , inahitaji mbele  ya  mashabiki  wa  nyumbani  kutofungwa  bao. Ireland ya  kaskazini , ni  ngumu katika  uwanja  wake  wa  nyumbani , amesisitiza Loew, "na hii inakuwa  kitu  cha kufurahisha."

UEFA Europa League 2017/18 | TSG Hoffenheim vs. Sporting Braga | TOR Hoffenheim
Sandro Wagner anachukua nafasi ya Mario Gomez ambaye ni majeruhiPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Siku  ya  Jumapili , mabingwa  hao  watetezi  wa  kombe  la  dunia  Ujerumani  watajitupa tena  uwanjani  kupambana  na  Azerbaijan  mjini  Kaiserslauten.

Wachezaji  walioteuliwa  na  kocha  Loew  ni  pamoja  na  walinda mlango : Marc-Andre ter Stegen (FC Barcelona) Kevin Trapp (paris St. Germain) walinzi:

Jerome Boateng(Bayern Munich), Matthias Ginter(Borussia Moenchengladbach), Mats Hummels (Bayern Munich), Joshua kimmich (Bayern Munich) Shkodran Mustafi (FC Arsenal) Marvin Plattenhardt (Hertha BSC), Antonio Ruediger(FC Chelsea), Niklas Sule (Bayern Munich) Wachezaji wa  kati/ washambuliaji  Julian Brandt (Bayer Leverkusen) , Emre Can (FC Liverpool) , Jukian Draxler (Paris St. Germain) Leon Goretzka (Schalke 04) , Toni Kroos (Real Madrid), Thomas Mueller (Bayern Munich) , Sebastian Rudy (Bayern Munich ) , Leroy sane (Manchester City) , Lars Stindl (Borussia Moenchengladbach) , Sandro Wagner (1899 Hoffenheim) , Timo Werner (RB Leipzig), Amin Younes (Ajax Amsterdam)