1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lisbon.Solana na Larijani wafungua njia ya majadiliano zaidi.

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBov

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana amesema kuwa mazungumzo yake na mkuu wa majadiliano ya kinuklia wa Iran Ali Larijani mjini Lisbon yalikuwa ya mafanikio.

Kabla ya mkutano huo , amesema kuwa hakutarajia kupata hali ya kufunguka njia.

Duru nyingine ya mazungumzo imepangwa kufanyika katika muda wa wiki tatu zijazo.

Marekani, Uingereza, Russia, Ufaransa, Ujerumani na China zinajadili vikwazo vya tatu vya umoja wa mataifa dhidi ya Iran kutokana na shaka kuwa nchi hiyo inajaribu kujenga silaha za kinuklia.

Muswada uliotayarishwa na Uingereza kwa ajili ya azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa linajumuisha vikwazo vya kusafiri, kuzuwia akaunti za benki pamoja na ukaguzi wa meli za mizogo za Iran pamoja na ndege.

Iran imesema kuwa mpango wake wa kinuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani.