1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON:Mugabe kualikwa kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Ulaya na Afrika

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BG

Ureno imetangaza kwamba itamualika rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kuhudhuria kikao cha pili cha mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika mwezi Desemba mjini Lisbon.

Kwa mujibu wa Afisa wa Ureno mualiko huo utatolewa katika siku chache zijazo.

Hapo jana Uholanzio ilisema itapinga hatua yoyote ya kualikwa kwenye mkutano huo rais huyo wa Zimbabwe.Wiki iliyopita waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown alisisitiza kwa mara nyingine kwamba nchi yake haitahudhuria mkutano huo ikiwa kiongozi huyo ataalikwa.

Hata hivyo ikiwa rais Mugabe atahudhuria mkutano huo atakuwa amekiuka kikwazo cha usafiri kilichowekwa dhidi yake na mataifa ya Ulaya.