1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON. Idadi ndogo yajitokeza kupiga kura ya maoni

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCT1

Wapiga kura nchini Portugal wamethibitisha kuwa wanataka mabadiliko katika sheria ya utoaji mimba nchini humo.

Matokeo ya kura ya maoni ya hapo jana yameonyesha kuwa asilimia 60 ya wapiga kura wanapendelea mabadiliko katika sheria hiyo dhidi ya asilimia 40 ya watu wasiopendelea mabadiliko hayo.

Hata hivyo idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza imeathiri mabadiliko hayo kwani hayataweza kugeuzwa na kuwa sheria.

Waziri mkuu wa Portugal Jose Socrates amesema atapitisha mswaada wa kubadili sheria japo kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo na kushindwa kuifanya sheria hiyo ipitishwe moja kwa moja.

Mabadiliko hayo yanahusu kuruhusiwa wanawake kutoa mimba hadi ya wiki kumi.

Portugal ni nchi ya kikatoliki na ilikuwa na sheria kali zaidi zinazohusu utoaji mimba katika jumuiya ya umoja wa nchi za ulaya.