1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LILONGWE:Upinzani wasusia majadiliano bungeni

15 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYv

Bunge nchini Malawi linaanza vikao vyake kujadili bajeti ya mwaka bila upande wa upinzani.Upinzani nchini humo unasusia kikao hicho kufuatia mzozo na chama tawala jambo linalo hatarisha upataji wa misaada nahuduma muhimu.Mjadala huo ulipaswa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni ili kuwezesha bajeti ya nchi hiyo kuanza kufanya kazi.Mazungumzo yalikwama mwezi jana kufuatia madai ya vyama vya upinzani kuwa chama tawala kinapora wanachama wake.

Rais Bingu wa Mutharika alitisha kulivunja bunge hapo jana endapo wabunge hawataanza majadiliano katika kipindi cha siku mbili zijazo.Spika wa bunge Louis Chimango aliwaagiza wabunge kuanza vikao hapo jana.Wanachama wa upinzani walikaa kimya bungeni kwani wanasusia majadiliano hayo mpaka mzozo huo utatuliwe.