1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LILONGWE:Kiongozi mpya wa kitengo cha kuendesha mashtaka ateuliwa

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1V

Malawi imeteua kiongozi mpya wa katika kitengo cha kuendesha mashtaka kinachozongwa na ufisadi. Alexious Nampota ndiye kiongozi mpya wa DPP baada ya viongozi wawili waliomtangulia kufukuzwa kazini na Rais Bingu Wa Mutharika wa Malawi kwa madai ya ufisadi.

Kiongozi huoy mpya anasisitiza kuwa kupambana na rushwa ni jambo muhimu kwa kitengo hicho.

Rais Mutharika alimteua Nampota mwezi jana ili kuchukua nafasi ya Tumalisye Ndovi aliyeachishwa kazi baada ya kuhusika na rushwa.Rais Mutharika anayeongoza chama kilicho na uwakilishi mdogo bungeni ana haki ya kumteua kiongozi yoyote wa kitengo hicho ila uteuzi huo sharti uidhinishwe na kamishna wa polisi,Tume ya Sheria aidha tume ya PAC iliyo na wapinzani wengi.