1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lewandowski aipa Bayern ushindi rahisi

Bruce Amani
8 Desemba 2016

Robert Lewandowski alifunga bao maridadi kabisa kwa njia ya free kick na likatosha kuwapa Bayern ushindi dhidi ya Atletico Madrid

https://p.dw.com/p/2TwkL
UEFA Champions League Bayern München vs. Atletico Madrid
Picha: Reuters/M. Rehle

Bayern Munich 1-0 Atletico Madrid 
(Lewandowski 27')

Bayern Munich wametua salama salimini katika hatua ya kumi na sita za mwisho za ligi ya klabu bingwa Ulaya, UEFA Champions League kwa mwaka wa tisa mfululizo baada ya ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya vinara wa kundi lao Atletico Madrid.

Mkwaju wa free kick wake Lewandowski ulitosha kuwapa Bayern ushindi huo wakati vijana hao wa kocha Carlo Ancelotti wakilipiza kisasi kichapo chao cha bao moja kwa sifuri mjini Madrid.

Ancelotti alifanya mabadiliko matano kwa kikosi chake kilichocheza mwishoni mwa mwiki katika Bundesliga. Joshua Kimmich, Javi Martinez, Philipp Lahm na Franck Ribery waliachwa nje na kuwapisha Rafinha, Juan Bernat, Renato Sanches, Arturo Vidal na Douglas Costa wakati Bayern waliutumia mfumo wa 4-3-3.

Matokeo mengine ya Champions League, Desemba 6. 

Basel 1-4 Arsenal

Paris SG 2-2 Ludogorets      

Benfica 1-2 Napoli

Dynamo Kiev 6 -0 Besiktas     

Manchester City 1-1 Celtic

Barcelona 4-0 Borussia Moenchengladbach     

PSV Eindhoven 0-0 Rostov

Mwandishi: Bruce Amani/DW
Mhariri: Daniel Gakuba