1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LANGKAWI:Zambia yatoa wito nchi kuchangia jeshi la kulinda amani Darfur

7 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbJ

Zambia imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchangia askari katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda kwenye jimbo lenye mzozo la Darfur.

Akizungumza nchini Malaysia, pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, Asia na Caribbean, Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Mundia Sikatana ametaka kupelekwa haraka kwa kikosi hicho.

Wiki iliyopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilidhinisha azimio la kupelekwa kikosi cha wanajeshi na poilisi 26,000 kulinda amani katika eneo hilo.

Viongozi wa makundi ya waasi wa Darfur nao walikutana mjini Arusha nchini Tanzania chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuzungumzia jinsi ya kutafuta amani katika eneo hilo.

Hata hivyo inaarifiwa ya kwamba Serikali ya Sudan haina shauku yoyote na yale yaliyokubaliwa na waasi.