1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAHORE: Benazir Bhutto aandaa maandamano mjini Islamabad

11 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJu

Kiongozi wa upinzani nchini Pakistan, Benazir Bhutto, anaandaa maandamo makubwa mjini Islamabad keshokutwa Jumanne kupinga hali ya hatari iliyotangazwa na rais Pervez Musharaf.

Bi Bhutto amelakiwa na mamia ya wafuasi wake waliopeperusha bendera za rangi nyeusi, nyekundu na kijani, ambazo ni rangi za bendera ya chama chake cha Pakistan People´s Party, wakati alipowasili mjini Lahore hii leo.

Benazir Bhutto anataraji kuongoza msafara wa magari mjini Islamabad Jumanne ijayo kumshinikiza rais Musharaf ajiuzulu wadhifa wake jeshini, amalize hali ya hatari aliyoitangaza wiki iliyopita, arejeshe katiba ya nchi na awaachie huru mawakili na wapinzani.

Polisi nchini Pakistan wameapa kuzuia msafara huo.