LAGOS: Spika wa Bunge ashinikizwa kujiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 29.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS: Spika wa Bunge ashinikizwa kujiuzulu

Msemaji wa Bunge la Nigeria amepinga wito wa vyama vya upinzani wa kumtaka ajiuzulu kuhusika na kashfa ya kandarasi.Patricia Olubunmi Etteh amesema,ripoti ya halmashauri maalum ya wabunge iliyondwa kuchunguza kandarasi zilizotolewa na spika huyo,ni kampeni iliyochochewa na chuki. Makundi ya upinzani yamezidi kupaza sauti yakimtaka Etteh ajiuzulu,kufuatia ripoti ya Jumatano iliyosema kuwa mbunge huyo hakufuata utaratibu unaotakiwa,alipotoa kandarasi za kufanyia ukarabati nyumba ya serikali anayoitumia na ile ya msaidizi wake.Ripoti hiyo imesema, kazi hiyo haikutangazwa kabla ya kutoa kandarasi za ukarabati.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com