1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lagos. Rais aonya dhidi ya wizi wa kura.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8j

Rais Olusegun Obasanjo ametoa wito wa kupambana na wizi wa kura kabla ya uchaguzi muhimu wa rais kesho Jumamosi baada ya kampeni zilizoambatana na ghasia na machafuko ya kisiasa.

Nigeria ikiwa ni nchi ya kwanza kwa utoaji mafuta barani Afrika imekuwa ikitolewa miito na jumuiya ya kimataifa kuzuwia ghasia za uchaguzi na Obasanjo amesema katika hotuba kwa taifa hilo leo , kuwa dunia inaiangalia Nigeria na hatupaswi kujikatisha tamaa.

Lakini kiasi cha watu 21 wameuwawa katika ghasia zinazohusika na uchaguzi katika siku baada ya uchaguzi wa magavana na mabaraza ya majimbo wiki iliyopita na Obasanjo amekiri kuwa uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu.

Vyama vikuu vya upinzani nchini Nigeria ambavyo hapo kabla vilitishia kususia uchaguzi wa hapo kesho vimekubali kushiriki.

Mpambano wa uchaguzi utakuwa kati ya wagombea watatu maarufu, Umaru Yar’Adua wa chama tawala cha Peoples Democratic PDP , makamu wa rais Atiku Abubakar na mtawala wa zamani wa kijeshi Muhammadu Buhari.