1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lagarde kuongoza IMF

Halima Nyanza29 Juni 2011

Waziri wa fedha wa Ufaransa, Christine Lagarde amechaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza kuliongoza Shirika la fedha la kimataifa -IMF.

https://p.dw.com/p/11l7i
Christine LagardePicha: dapd

Bodi ya watendaji ya shirika hilo, yenye wajumbe 24,  imesema jana kwamba Lagarde mwenye umri wa miaka 55, ataanza kutumikia awamu ya kwanza ya miaka mitano, kuanzia Julai 5.

Christine Lagarde kandidiert für IWF Posten
Waziri wa Fedha wa Ufaransa, Christine LagardePicha: AP

Bibi Lagarde amechukua nafasi ya Mkurugenzi mtendaji wa zamani Dominique Strauss Kahn, ambaye alijiuzulu mwezi Mei, kutokana na tuhuma za kumbaka mhudumu mmoja wa hoteli, mjini New York, Marekani.