1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumbukumbu ya miaka kumi tangu kufariki kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

14 Oktoba 2009

Leo ni miaka 10 tangu kufariki dunia Rais wa kwanza wa Tanzania na mmoja kati ya waliokuwa viongozi mashuhuri barani Afrika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

https://p.dw.com/p/K63z
Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere wa TanzaniaPicha: DPA

Marehemu Nyerere hata hivyo ameacha maoni ya mchanganyiko kuhusu utawala wake wa kijamaa na msiamamo wake katika masuala ya Afrika na kimataifa. Pamoja na hayo moja kati ya mafanikio yake makubwa ni mchango uliotolewa na nchi yake katika ukombozi wa bara la Afrika .Nimezungumza na Mwenyekiti wa wakfu wa Mwalimu Nyerere Dr Salim Ahmed Salim aliyewahi kuwa Waziri mkuu wa Tanzania na baadae katibu mkuu wa uliokuwa umoja wa nchi huru za Afrika OAU, na kwanza anaelezea jinsi Mwalimu Nyerere anavyokumbukwa .