1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

kudhibiti silaha za nuklia kuna matumaini gani ?

14 Aprili 2010

Mkutano wa Obama wa kudhibiti nuklia

https://p.dw.com/p/Mw1x
Obama na vipi kudhibiti nuklia ?Picha: AP

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani, leo wamechambua mada mbali mbali -na usoni kabisa, ni mapendekezo mapya ya kodi za mapato nchini na mkutano aliouitisha Rais Obama, mjini Washington, wa kudhibiti silaha za nuklia ulimwenguni .

Gazeti la Mannheimer Morgen, kuhusu mkutano wa kilele juu ya silaha za atimoki laandika:

"Kwa mkutano wake mkubnwa aliouitisha ,Rais Obama, alao amefaulu kuufanya ulimwengu umepiga hatua mbele katika kuzindukana na hatari isiodhibitika ya kuenezwa na kurundika bila hadhari za kutosha, silaha na miale ya kinuklia.Lakini bado kuna njia ndefu ya kwenda hadi kuanzia ahadi zilizotolewa kugeuka mapatano ya kimataifa yatakayo ziwajibisha nchi zote.

Muda alioweka shabaha rais Obama, ni wa matumaini mkubwa mno.Mkutano wake lakini , ni hatua ya kwanza ya kutia moyo. Kuwa imesadifu dola la nuklia nambari 1, ambalo ndilo dola pekee duniani kuwahi kuripua bomu la nuklia,kunasisitiza juhudi hii muhimu inayoongoza."

Likiendeleza mada hii,gazeti la Der Neue Tag, linaandika kwamba, usalama wa kimataifa chini ya misingi ya kisheria, kama vile Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani anavyodai, au kuwapo misngi maalumu inayo yawajibisha mataifa yote jinsi ya kutumia zana za nuklia, ni hatua ya kwanza kwenda njia ilionyoka.Gazeti lauliza:

"Mbona ni mataifa 50 tu, yalioitikia mwaliko wa rais Obama kwenda Washington ,mji mkuu wa Marekani ? Kwani, tani alfu kadhaa za nishati ya kinuklia ambazo kwa kupita miaka mingi zimeletwa duniani na kuenezwa ,zinatosha kuunda mabomu alfu kadhaa ya atomiki lakini pia hata mabomu machafu-(dirty bombs)."

Ama gazerti la Nordbayerischer Kurier, linaandika kwamba, hakuna ajuwae iwapo magaidi tayari wana uwezo kuunda mabomu hayo machafu kutokana na zana za nuklia ?

Ni madhumuni basi ya rais Obama kwa mkutano wake huo wa kilele mjini Washington, kuuzindua ulimwengu juu ya hatari kama hizo. gazeti laongeza:

"Kwa bahati mbaya ,mada kama hizi muhimu zina washughulisha tu wale wenye hamu nazo.Hatuwezi kufanya lolote ili kupunguza hatari ,wanadai wengineo na wanaendelea kucheza na moto."

Gazeti la "MÄRKISCHE ALLGEMEINE" linachambua mapendekezo ya kodi za mapato yaliotolewa na chama cha kiliberali cha FDP katika serikali ya muungano ya Ujerumani.Gazeti laandika:

"Pole pole, chama cha FDP kinaamka usingizini na kuutambua ukweli wa hali ya mambo.Wakati muda mfupi tu nyuma, chama hiki cha kiliberali kiliwaahidi wapigakura kuwapunguzia mno malipo ya kodi, sasa chabainika kimerudi mno nyuma.Hatua hii yafaa kukaribishwa na yamkini, ikatengeza hali ya hewa ndani ya serikali ya muungano ya Ujerumani.

Hatahivyo, linabaki swali la kuulizwa:Kutokana na kasoro kubwa iliopo katika bajeti ya serikali,vipi kupunguzwa kodi kidogo za mapato kunaweza kugharimiwa ? "

Mwandishi: Ramadhan Ali/DPA

Mpitiaji:Abdul-Rahman,Mohammed