1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUALA LUMPUR: Mitambo mitano mikuu ya nyuklia imefungwa

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhT

Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa-IAEA limethibitisha kuwa Korea ya Kaskazini imefunga mitambo yake mikuu mitano ya nyuklia. Mkuu wa IAEA,bwana Mohamed El-Baradei alipozungumzwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika mji mkuu wa Malaysia,Kuala Lumpur alithibitisha habari hizo na akaonya kuwa hii ni hatua ya mwanzo tu katika majadiliano yalio magumu.

Wakati huo huo,maafisa kutoka madola sita wameanzisha tena majadiliano yao yanayohusika na kusitishwa kwa mradi wa silaha za nyuklia wa Korea ya Kaskazini.Mjumbe wa Marekani,Christopher Hill amesema,ni matumaini yake kuwa wakati wa majadiliano ya juma hili kutapatikana mpango wa kusitisha mradi unaohusika na silaha za nyuklia.