Kosovo na uhuru | NRS-Import | DW | 04.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Kosovo na uhuru

Jimbo la Kosovo lajiandaa mwezi huu kujitangazia uhuru kama ilivyoahidi

default

''Rais Boris Tadic anasema anatoa kipaumbele kwa suala la kujiunga na umoja wa Ulaya''

Maafisa wa ngazi za juu wa Jimbo la Kosovo lililojitenga na serbia wamesema watajitangazia uhuru wa jimbo hilo hivi karibuni ikiwa ni  siku moja baada ya kufanyika uchaguzi wa rais uliomrudisha madarakani   rais Boris Tadic anayeungwa mkono na nchi za magharibi.


Siku moja baada ya uchaguzi wa rais nchini Serbia spika wa bunge la jimbo la Kosovo Jakup Krasnici amewaambia waandishi wa habari  mjini Pristina kwamba wako tayari kwa ushirikiano na washirika wao wa nchi za Magharibi,Marekani na Umoja wa ulaya kutangaza uhuru wa jimbo la Kosovo mwezi huu.

Uongozi wa jimbo hilo la Kosovo unaowakilishwa na idadi ya asilimia 90 ya waalbania unasubiri kwa hamu kubwa kujitanngazia uhuru kamili kutoka kwa Serbia ambayo bado inaudhibiti wa jimbo hilo.Rais Boris Tadic anayeegemea upande wa nchi za magharibi alichaguliwa tena madarakani dhidi ya mpinzani wake kutoka upande wa kizalendo mwenye msimamo mkali Tomislav Nikolic.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema  hakuna shaka kwamba ni bora zaidi kwa ushindi huo wa Boris na hasa kwa upande wa jumuiya ya kimataifa kuelekea suala la uhuru wa jimbo la Kosovo.Hata hivyo hali katika Serbia ni ya  mashaka mno kufuatia kugawika kwa jamii nzima ya taifa hilo hali ambayo wachambuzi wa mambo wanasema ikasababisha zaidi mzozo katika serikali.Umoja wa Ulaya umekaribisha kwa moyo mkunjufu matokeo ya uchaguzi wa rais ambao umetajwa kuwa  kama ni kura ya maoni juu ya vipi Serbia inapasa kuangalia  suala kutaka kujitangazia uhuru kwa jimbo la Kosovo.Javier Solana ni Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya...otone


Baada ya ushindi wake Rais Tadic amesema jambo muhimu katika agenda zake ni kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya wakati mpinzani wake Nicolic akilemea zaidi upande wa Urussi ambayo imekuwa ikiiunga mkono Serbia dhidi ya uhuru wa jimbo la Kosovo.Wadadisi wa mambo wanasema ushindi wa rais Boris umeonyesha ni jinsi gani miaka saba baada ya kun'golewa madarakani kwa Milosevic waserbia walivyogawika sawia kati ya wazalendo wenye msimamo mkali na wale wenye mtizamo wakinadharia wanaogemea nchini za Magharibi.Wakati rais Boris akiwataka waserbia wajitaarishe kuingia katika Umoja wa Ulaya japo kwa machungu ya kuipoteza Kosovo waziri mkuu  Vijislav Kostunica ambaye anatokea katika chama kinachounda muungano wa chama tawala cha rais Boris haungi mkono kuchaguliwa tena kwa rais Boris huku akitaka pawepo msimamo mkali juu ya hatua ya kutangaza uhuru kwa jimbo la Kosovo,aidha anapendekeza vikwazo vya kidiplomasia dhidi ya mataifa ya magharibi pamoja na kuukana Umoja wa Ulaya na hatua za kulibana jimbo hilo kiuchumi.Msimamo huo wa waziri mkuu unatajwa na wachambuzi wa siasa kuwa ni dalili ya kuelekea kuvunjika kwa muungano unaotawala ambapo huenda chama cha Tadic cha Demoratic Party  kikatishia uchaguzi wa mapema wa bunge na Kustunia nae akatishia kuunda serikali na chama cha wazalendo cha Nikolic aliyeshindwa katika uchaguzi wa rais.►◄

 • Tarehe 04.02.2008
 • Mwandishi Ramadhani Yusuf, Saumu
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D2GW
 • Tarehe 04.02.2008
 • Mwandishi Ramadhani Yusuf, Saumu
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D2GW

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com