1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yatishia vyombo vya habari vya Kigeni

Saumu Mwasimba
15 Novemba 2016

Umoja wa Mataifa una wasiwasi juu ya sheria mpya kuhusu vyombo vya habari vya kigeni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo vimetakiwa kurusha matangazo yao chini ya vituo vya ndani vinavyokubalika

https://p.dw.com/p/2SiRp
DR Kongo | Archivbild Radio Okapi in Kinshasa
Mtangazaji Dunia MukundaPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

 Baada ya kuchukuwa hatua dhidi ya vituo viwili maarufu vya redio nchini humo serikali ya Kongo imeanzisha sheria mpya kuelekea vyombo vyote vya habari vya kigeni vinavyotangaza katika nchi hiyo.Na tayari waziri anayehusika na masuala ya habari Lambert Mende ametoa muda wa siku 30 sheria hiyo kutekelezwa.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inataka kwa siku zijazo kuzuia matangazo yote ya redio za kigeni nchini humo ikiwemo Deutsche Welle na shirika la habari la uingereza BBC.Waziri wa nchi hiyo anayehusika na masuala ya habari Lambert Mende akizungumza hapo jana Jumatatu alisema kwamba vituo vya habari vya kigeni vimekuwa chachu ya kuwapa nguvu wapinzani.

Amefafanua zaidi kuhusu sheria mpya ya serikali kuelekea matangazo ya vyombo vya kigeni na kubaini kwamba kwa muda wote redio hizo zitakapokuwa zinatangaza zitalazimika kutangaza kupitia  washirika wa redio za ndani zinazokubalika.Yote hayo kwa mujibu wa waziri Mende yanabidi kuzingatiwa ndani ya kipindi cha siku 30 zijazo.

Joseph Kabila Präsident Demokratische Republik Kongo
Rais Joseph KabilaPicha: Getty Images/AFP/T. Mianken

Vituo vya habati ambavyo ni miongoni mwa vinavyolengwa na sheria hiyo ni pamoja pia na kituo cha redio cha Ufaransa RFI na kituo cha televisheni cha TV5 Monde.Kimsingi wapinzani katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wapinzani wanahisi  kupata nafasi zaidi ya kusikika kuliko katika redio za kigeni kuliko  ilivyo katika vyombo vya ndani vinavyodhibitiwa na serikali.Wapinzani wanamtaka rais Kabila aondoke madarakani  pindi muhula wake utapomalizika mwezi Desemba mwaka huu.

Hatua hiyo ya serikali ya Kongo bila shaka imeutia wasiwasi umoja wa Mataifa ambapo  ujumbe wa baraza la usalama la Umoja huo uliokuweko Kongo tangu siku ya Ijumaa ulitowa tamko kupitia kiongozi wake Alexis Lamek ukisema sheria hiyo inatia mashaka na kwa hakika Kongo haifuati njia sahihi ila inachokifanya ni kupitia hatua hiyo ni kujenga hali ya kutoaminika katika wakati huu muhimu kabisa.

Waziri wa habari Lambert Mende ameweka wazi kwamba chombo chochote cha kigeni kitakachoshindwa kufuatia sheria iliyowekwa ndani ya siku hizo 30 kitachukuliwa hatua.Kwa maana hiyo haijawa wazi ni hatua gani hasa zitavikabili vyombo vya kigeni vinavyotangaza katika nchi hiyo kama Deutsche Welle Bbc,au Sauti ya Amerika Voa.

Demokratische Republik Kongo - Ausschreitungen in Kinshasa
Wapinzani hawapewi nafasi ya kusikika katika Redio za ndaniPicha: Getty Images/AFP/J. D. Kannah

Tayari kituo cha redio cha Umoja wa Mataifa nchini humo Redio Okapi kilichopo Kinshasa kimeshafungiwa tangu wiki moja sasa na Frikwensi ya matangazo ya RFI mjini Kinshasa na Lubumbashi zimefungwa kabisa. Kwa hivi sasa kuna kiasi vituo 30 vya redio vya ndani ya nchi hiyo ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambavyo kando ya matangazao yao wanarusha pia matangazo ya Deutsche Welle.Lakini katika kipindi kifupi kijacho mambo huenda yasiwe kama yalivyo na hivyo basi itatakiwa kuwa na kibali maalum kutoka wizara ya habari kuruhusiwa kusikika Kongo na pengine katika siku zijazo vyambo vya kigeni huenda vikalazimika hata kuwa na mtu maalum anayetambulika rasmi nchini Kongo kusimamia matangazo yao.

Mwandishi:Christine Harjes/Saumu Mwasimba/ (dpa)

Mhariri :Gakuba Daniel