1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano la "jukwaa" la vyombo vya habari laanza

25 Juni 2012

Kongamano linalojulikana kama Global Media Forum ambalo linawaleta pamoja wataalamu kutoka vyombo vya habari, wanasayansi na wanasiasa, limeanza leo Jumatatu (Juni 25 hadi 27 ) katika jengo la Deutsche Welle mjini Bonn

https://p.dw.com/p/15Kpp
Afghanische Schülerinnen und Schüler bei der Abiturprüfung

" Elimu bado ni mada kuu katika suala zima la utandawazi," alitamka hayo Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle, Erik Bettermann. Jinsi gani " Elimu kwa wote" lilivyo jambo muhimu, ndiyo suala kuu la majadiliano ya siku tatu miongoni mwa wataalamu kutoka vyombo vya habari, wanasayansi na wanasiasa kuanzia Jumatatu (Juni 25 hadi 27 ) katika kongamano linalojulikana kama Global Media Forum katika jengo la Deutsche Welle mjini Bonn." Habari na elimu ndiyo msingi wa harakati za chombo cha matangazo ya kigeni cha Ujerumani", anasema Mhariri mkuu wa DW, Ute Schaeffer.

Kwa mujibu wa idadi rasmi ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa mataifa, kiasi ya watu 800 milioni hawajui kusoma na kuandika.Wakati huo huo, inaelekea Ulimwengu ni jamii ya habari, ambayo kwa mujibu wa Erik Bettermann,hutupa nafasi ya kupata maarifa kila wakati na popote tulipo.

Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Welle Erik Bettermann
Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Welle Erik Bettermann

Vyombo vya habari kutoa mwangaza
Ni kwa sababu hii hasa, vyombo vya habari kote duniani vinawajibu. " Vina jukumu muhimu kama chombo cha kutoa muwangaza ", anasisitiza Mkurugenzi mkuu wa DW. Kwa watu wa tabaka mbali mbali katika Dunia ya utandawazi, elimu, utamaduni na elimu kwa wote, yanaweza kuwa ni ufunguo wa kuweza kuishi pamoja kwa amani, kwa maendeleo na majadiliano baina ya watu wa tamaduni mbali mbali.

Katibu mkuu wa Tume ya Ujerumani ya Shirika la UNESCO , anakubaliana na msimamo huu:" Uhuru wa magazeti, ubora wa elimu na mchanganyiko wa tamaduni, ni mambo muhimu kwa ajili ya kuwa na jumuiya huru na zenye nguvu. Mwaka huu Tume ya Ujerumani ya Shirika la UNESCO,imechukua nafasi ya kuwa kinara ya mkutano wa Bonn.

Miongoni mwa wageni maarufu katika kongamano la Global Media Forum kawa mara ya kwanza ni Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle. Anazungumzia juu mchango wa ushirikiano na maajadiliano katika Dunia ya utandawazi. Pia anatarajiwa Rais wa zamani wa Indonesia Jusuf Habibie.

Misimamo ya Sayansi duniani

Thomas Pogge, profesa wa falsafa ya siasa na masuala ya kimataifa katika chuo kikuu cha Yale, New Haven (Marekani) na Franz Josef Radermachaer, profesa wa sayansi ya kompyuta katika chuo kikuu cha Ulm na mwanachama wa kilabu ya Roma, wataelezea wazi misimamo ya sayansi katika hali ya dunia na hivyo kuwasilisha maelezo ya kutosha kwa ajili ya majadiliano. Lakini zaidi ya watu wengine 50 katika hafla hiyo-walioandaliwa na mashirika na makampuni ya kitaifa na kimataifa , watatoa maoni mengi tofauti: UNESCO imetambuwa kuwa mchanganyiko wa tamaduni ni chachu kwa hali endelevu katika kanda ya Ulimwengu wa Kiarabu.

Mada kuu ya kongamano hilo mwaka huu ni Elimu kwa wote
Mada kuu ya kongamano hilo mwaka huu ni Elimu kwa wotePicha: Fotolia/Living Legend

Shirika la Ujerumani la kubadilishana wasomi (DAAD), linajishughulisha na suala la kama vyuo vikuu vinaweza kuwa chombo cha mabadiliko. Elimu ya haki za binaadamu na maamuzi binafsi ya kijinsia ni mada inayozingatiwa na taasisi ya Ujerumani ya haki za binaadamu (DIMR) na Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa (GIC) na Taasisi ya Maendeleo ya Ujerumani (DIE), zinafafanua juu ya mchango wa mdahalo baina ya tamaduni mbali mbali kwa changamoto za " utawala bora".

"Kwa hiyo sisi si mkutano wa vyombo vya habari si mkutano wa kisiasa wala mkutano wa kisayansi," anasema Meneja wa GMF Ralf Nolting, bali ni watu tuliokusanyika katika meza moja , kutathmini nini suluhisho la matatizo ya dunia." Kinachofaanana kwetu sote ni imani ya kwamba vyombo vya habari vimetoa mchango muhimu katika kutambua suluhisho la matatizo na mawasiliano. Kutokana na hayo ndiyo maana kuna Kongamano hili la Global Media Forum- ambalo sasa linafanyika kwa mara ya tano- likiwa ni jambo la mafanikio , anasema Nolting.

Mwandishi: Mast-Kirschning,Ulrike/ Mohammed Abdul-Rahman

Mhariri:Josephat Charo