1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la vijana la Afrika laendelea Ruanda.

23 Januari 2009

Nani ataibuka bingwa Kigali ?

https://p.dw.com/p/Gf1f
Mashabiki wa Manchester CityPicha: picture-alliance/ dpa

Kombe la Afrika la vijana chini ya umri wa miaka 20, linaendelea leo huko Ruanda-Robinho wa Brazil aomba radhi kwa klabu yake ya Manchester City.

Mshambulizi wa Ufaransa Nicholas Anelka anadai klabu za Uingereza katika champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulay, zitatamba mbele ya zile za Itali.

Kombe la vijana la Afrika chini ya umri wa miaka 20,linaendelea nchini Ruanda zikishiriki timu kama mabingwa mara 5 Nigeria,simba wa nyika Kamerun, Misri,Black Stars-Ghana na hata Afrika Kusini.Afrika Kusini inaendelea kutamba baada ya kuilaza Nigeria 2:1.hata wenyeji Ruanda hawajakata tamaa.

Ama katika dimba barani ulaya, Premier League inapumzika mwishoni mwa wiki hii na kukiachia kinyanganyiro cha Kombe la FA:

Manchester United iliotwaa uongozi wa Ligi mwishoni mwa wiki iliopita ilipoipiku Liverpool,inacheza leo Tottenham Hotspurs wakati Potsmouth wana miadi na Swansea. Mahasimu wao Manchester katika kuania ubingwa wa Uingereza-Chelsea, wanacheza leo nyumbani na maadui zao ni Ipswitch Town. Wolverhampton wanderes wanacheza na Middlesbrough.

Kesho jumapili, itakua zamu ya Arsenal kuitembelea Cardif City.Liverpool ina miadi pia kesho na Everton.

Upande wapili wa mpaka, Olympique Lyon inacheza leo na Concarneau katika kundi la timu 32 zilizosalia kuania kombe la shirikisho la dimba la Ufaransa.Stade Rennes inapambana na St.Etienne.

Seriea A-ligi ya itali, inaendelea huku Reggina ikiwa na miadi na Chievo.

Juventus inapapurana na Fiorentina.

Kesho itakua zamu ya ya Bolognia kutembelewa na AC Milan wakati mahasimu wao Inter Milan wanawakaribisha nyumbani Sampdoria. Siena iko pia nyumbani ikiwa na miadi ya kutekeleza na Udinese.

Napoli inacheza na AS Roma.

Nchini Spain, Villa Real wana miadi leo katika la Liga na Osasuna huku viongozi wao wa Ligi FC Barcelona wanachuana na Numancia.

Kesho ni zamu ya Getafe kuoneshana na Sporting Gijon na Malaga na Atletico Madrid.

Real Malloca wanacheza na Valencia.Espanyol itafunga safari kucheza na Real Valladolid.

Tukisalia katika dimba la Uingereza,kocha wa Manchester city Mark Hughes

amesema kwamba stadi wao kutoka Brazil, robinho ameomba radhi kwa kuondoka katika kambi ya mazowezi huko Tenerife bila ya ruhusa.Pia alikanusha taarifa kuwa Robinho atabadilishwa na jogoo la chelsea muivory Coast Didier Drogba Januari hii.

Robinho aliruka kwa ndege kwenda nyumbani Santos,Brazil na amesema ni kwa shughuli ya dharura ya familia. Hii iliwakasirisha viongozi wa Manchester City waliodai stadi huyo wa Brazil achukuliwe hatua ya nidhamu akirejea kutoka Brazil.Hughes alikanusha kuwa kuondoka kwa Robinho kulihusiana na kuporomoka mpango wa kumuajiri mbrazil mwenzake Kaka kutoka AC milan, nchini Itali na akihisi kwamba mipango mikubwa ya Manchester city,haitatimilia.

Kaka alikuwa ajiunge na Manchester city kwa kitita cha dala milioni 150-ambacho ni rekodi.AC milan iliweka wazi kwamba haimuuzi Kaka.

Hughes, mshambulizi wa zamani wa Manchestrer United na Chelsea, alikanusha kuwa Robinho alikaribia kujiunga na Chelsea.

hivi sasa robinho amesisitiza utiifu wake kwa Manchester City alipoandika katika mtandao wake kuwa ana usuhuba mzuri bado na kocha Mark Hughes.

Stadi mwengine wa Chelsea aliegonga vichwa vya habari kati ya wiki hii ni mfaransa Nicolas Anelka.Yeye amebashiri kwamba timu za Uingereza katika kombe la Ulaya-champions League zitatamba mbele ya maadui zao klabu za Serie A-Ligi ya Itali:

ANELKA alibashiri hivyo kwa ujeuri wakati wa mahojiano na gazeti la michezo la Itali:La Gazetta dello Sport.Chelsea anaoichezea Anelka ina miadi na Juventus ya Itali wakati mabingwa wa Ulaya na dunia Manchester United watakutana na viongozi wa ligi Inter Milan. Arsenal wamepangwa kucheza na AS Roma.

Anelka amezichezea timu 8 tofauti katika nchi 4 mbali mbali,lakini bado hakucheza Itali na hivyo licha ya kuwa mkewe ni muimbaji wa kitaliana Barbara Tausia. Anelka ambae wazee wake ni wa asili ya kisiwa cha Martinique,alifichua alikaribia mara mbili-tatu kuangukia katika Ligi ya itali.

Anelka ana sifa za kushinda vikombe vyote 2 huko Uingereza akiichezea arsenal,kombe la ulaya -champions League alipoichezea Real madrid ya Spian na taji la uturuki alipovaa jazi ya Fenerbahce.Anelka alitawazwa mabingwa wa ulaya na Ufaransa mwaka 2000 walipoishinda Itali katika finali.Kwa bahati mbaya Nicholas Anelka hakuwamo katika ile timu ya Ufaransa iliotwaa kombe la dunia,huko huko Ufaransa,1998.

Ikiwa alivyobashiri Anelka, timu za Uingererza zitatamba tena mbele ya Itali ni kweli, tusubiri tuone wiki zijazo.