Kombe la klabu bingwa Afrika | Michezo | DW | 16.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kombe la klabu bingwa Afrika

Kinyan'ganyiro cha Kombe la klabu bingwa barani afrika kinarudi uwanjani mwishoni mwa wiki huku klabu kadhaa zikiwa hatarini kupigw a kumbo.Timu za taifa pia zajinoa kwa tikiti za kwenda ghana mwakani.

Bundesliga-ligi ya Ujerumani iko uwanjani na Schalke, viongozi wa Ligi, watajua jumamosi hii hatima yao iwapo huu utakuwa msimu wao wa kutoroka na taji au watasregeza kamba na kuwaachia Bremen au Munich kutoroka na kombe tena.Wakiwa pointi 4 usoni,Schalke wamekuwa wakipepesuka hivi karibuni baada ya kupitisha mechi 4 bila ya ushindi.

Jumamosi basi wanaikaribisha nyumbani Stuttgart inayosimama nafasi ya 3 na firimbi ya mwisho hivi punde itaamua iwapo Schalke ina m atumaini tena ya ubingwa au la.Bremen iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi inakutana na Mainz hapo kesho.wiki iliopita ilimudu suluhu ya bao 1:1 na mabingwa Bayern Munich mjini Munich.

Mabingwa Bayern Munich, wanacheza wakati huu na Frankfurt inayotapatapa isizamishwe daraja ya pili ilikotoka.Timu hii ya kocha Ottmar Hitzfeld haikubarikiwa ushindi mwishoni mwa wiki i.liopita ilipoonana na Bremen,lakini leo mbele ya Frankfurt,bayern munich haitaachia tena pointi 3 ziitoroke.

Munich ikionesha kuridhika na jinsi kocha wao ottmar Hitzfeld anavyoiongoza timu,imemrefushia mkataba wake kwa m waka mzima.Kulikuwapo shauri la Michael Ballack anaeichezea Chelsea wakati huu, kuwa bora Munich ingemuajiri stadi wao wa zamani aliewaongoza kutwa kombe la Ulaya 2001,Stefan Effenverg aee kocha wao mpya.

Labda, Effenberg asingeweza kusikizana na meneja Uli Hoenes ambae hakukawia kumfugisha mkataba Ottmar Hitzfeld.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza,Manchester United imepania leo kuparamia kileleni mwa Ligi hiyo ya Uingereza ,mradi tu ikomoe Bolton Wanderers.Ikiwa pointi 9 usoni mwanzoni mwa wiki hii ,lakini 6 tu hivi sasa baada ya Chelsea kuizaba Manchester City bao 1:0 kati ya juma, Manchester lazima ijifunge kibwebwe uwanjani Old Trafford.Chelsea- mahasimu wao, wana mteremko wakicheza nyumbani na Shefield United.

Katika La Liga-Ligi ya Spain ikiwa timu 6 bora kabisa zimetengana kwa pointi 7 tu,nani atakimbia na taji haijulikani kwa sasa.Mechi 12 zikisalia ,Barcelona na sevilla zaongoza kwa pointi zao 50-pointi 3 zaidi kuliko Valencia.Real Madrid inafuata ikiwa na pointi 45-mbili zaidi kuliko Zaragoza na Atletico Madrid.

Timu kadhaa za taifa za Afrika zinajiwinda kwa changamoto za mwishoni mwa wiki ijayo za kuania tiketi za finali ya mwakani ya Kombe la Afrika la mataifa nchini Ghana:

Nigeria chini ya kocha wake mpya mjerumani Berti Vogts inajiwinda kwa zahama na Uganda.“hakuna shaka tunahitaji pointi zote 3 kutoka mpambano huu ili kukata tiketi yetu ya kombe la Afrika ,lakini shauku yangu haipo tu katika matokeo,natarajia pia mchezo mzuri wa timu yangu.“ –alisema Berti Vogts,alieiongoza Ujerumani katika Kombe la dunia 1994 huko Marekani na katika finali ya Kombe la Ulaya,Uingereza Euro 96.Nigeria ikiwa inaongoza kundi la 3 ina pointi 6 kutoka mechi zote 2 ,wakati mahasimu wao wakubwa kundi ni,Uganda Cranes wakiwa nyuma kwa pointi 2 tu.

Hivyo changamoto ya wiki ijayo itakua ya kusisimua kwa mjerumani Berti Vogts.Mara ya mwisho Nigeria kucheza na Waganda ilikua miaka 14 iliopita pale Super Eagles walipozimwa na kutoka sare tu 0:0 mjini Kampala.

Berti Vogts aliewasili Nigeria mapema wiki hii kabla ya mpambano na Uganda, Machi 24 amesisiza kuwa muhimu kabisa ni heshima,nidhamu na maandalio bora ili kufanikisha kazi yake ya ukocha nchini Nigeria.Niger na Lesotho, ni timu 2 nyengine katika kundi hili.

KOMBE LA CAF NA KLABU BINGWA:

Katika kinyan’ganyiro cha mwishoni mwa wiki hii cha kombe la CAF-kombe la shirikisho la dimba la Afrika,klabu 3 maarufu zaweza zikanyolewa bila ya maji na kupigwa kumbo nje ya mashindano:Moulaudia Alger ya Ageria na Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zinabidi kufuta mabao 3 zuilizochapwa katika duru ya kwanza.Na Al-Merreikh ya Sudan inapanda pia mlima baada ya kuzabwa na contonTchad wiki 2 nyuma.

Mouloudia ilikuwa timu ya kwanza ya Afrika kutwaa kombe hili 1976 walipofuta mabao 3 ya duru ya kwanza ya Hafia ya Guinea na kutoroka na kombe-mpambano ambao ulimkasirisha rais wa wakati ule wa guinea ahmad sekotoure na kumtimua hata waziri wake wa michezo.

Mouloudia ,moptema Pem,be,Merreikh,Ismailia ya Misri na Union Douala ya Kamerun pamoja na Sporttif Sfaxien ya tunisia ziliwahi kila moja kutoroka na kombe hilo la CAF.

Katika changamoto za Kombe la klabu bingwa, Zamalek mahasimu wa mabingwa nyumbani Al Ahly, wanakabiliwa na hatari ya kupigwa kumbo leo.Kati ya wiki walitolewa jasho na Al Ahly ya Saudia kabla haikuibuka kileleni mwa Ligi ya nchi za kiarabu na kujipatia tiketi ya nusu finali.

Zamalek kwahivyo, haikuwa na wakati wa kutosha wa kupumua kabla kuingia leo uwanjani kuumana na Al Hilal ya Sudan katika duru ya pili ya kombe la klabu bingwa mjini Cairo.

Mabingwa watetezi Al Ahly pia ya Misri hawna taabu ya kuingia duru ijayo baada ya kutoka sare 0:0 duru ya kwsanza na Highlanders ya zimbabwe .Ushindi wao huo ulipatikana licha ya kutocheza kwa mastadi wao wa kiungo Mohamed Barakat na Mohamed Aboutraika.

Asec ya Ivory Coast;Esperence ya Tunisia,TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo na Wydad Casablanca ya Morocco ndio mabingwa wa zamani wanaoingia uwanjani.

MBIO ZA MAGARI:

Bingwa wa mabingwa wa mbio za magari za fomular one:Michael Schumacher, atatumbua macho tu kesho msimu wa mwaka huu wa mbio za magari ukianza huko Melbourne,Australia.Na hii kwake, itakua mara ya kwanza tangu 1991.Hatahivyo, bingwa mara 2 Fernando Alonso hatojali kutoshiriki kwa Michael Schumacher kiboko yake.

Michael Schumacher amestaafu bada ya kuwa bingwa si chini yxa mara 7.