1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kombe la klabu bingwa Afrika kesho Cairo:

Duru ya 3 ya kinyan'ganyiro cha Kombe la Klabu Bingwa Afrika inaanza kesho mjini Cairo kwa changamoto kati ya mabingwa Al Ahly na mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.

Kesho firimbi Italia mjini Cairo,Misri kuanzisha duru ya tatu ya mwishoni mwa wiki hii ya kinya’nganyiro cha Kombe la klabu bingwa barani Afrika:Mabingwa Al Ahly wana miadi nyumbani na Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini katika marudio ya finali ya Kombe hili ya 2001.Beni McCathy atia bao lake la 20 msimu huu pale Blackburn ilipoipiga kumbo jana Watford kwa mabao 3:1.Na rifu wa ki-gambia apigwa na mashabiki wa Union Duala ya Kameroun baada ya kutoa mkwaju wa penalty dakika ya mwisho mjini Lagos.

Kwanza finali ya kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani mwezi ujao katika uwanja wa olimpik mjini Berlin,itakua kati ya Stuttgart ilioipiga kumbo hapo jana Wolfsburg na Nüremberg-timu 2 za kusini.

Kesho macho ya mashabiki wa dimba wa Afrika yataanza kukodolewa Cairo ambako mabingwa wa afrika Al Ahly watamteremsha tena uwanjani jogoo lao Mohamed Aboutraika kulibomoa lango la Mamelodi Sundowns katika kile wengine wakiona ni marudio ya finali yao ya 2001.Mwaka huo,Al Ahly ilitoka nyuma na kutoka suluhu bao 1:1 na Mamelodi nyumbani mwao Pretoria.Halafu mabao 3 ya Khaled Bibo yakaivalisha taji Al Ahly mjini cairo,uwanja ule ule kesho Al Ahly imekamata jembe kuichimbia Mamelodi kaburi lake jengine msimu huu.

Aboutraika ndie aliekua jogoo lililowika mwaka jana pale Al Ahly ilipoibuka timu ya tatu kutetea ubingwa wake kwa kuitimua Sporttif Sfaxien ya Tunisia katika finali.

Mara hii bendera ya Tunisia inapepewa na Esperence ambayo imefunga safari ndefu hadi Mwanza,Tanzania kujaribu kupiga msumari wa mwisho katika jeneza la young Africans.

Lakini Yanga ina matumaini gani ya kufuta mabao 3:0 nyumbani ?

Rifu kutoka gambia John Mendy, alikiona jana kile ,kilichomtoa kanga manyoya.Mashabiki wa Union Douala ya Kameroun walimtandika rifu huyo sawa sawa baada ya kutoa mkwaju wa penalty dakika ya mwisho dhidi ya timu yao huko Lagos,Nigeria walipocheza na Kwara United.Douala kwa mabao 4-3 ikatolewa nje ya kombe la CAF.Hadi dakika hiyo,Unioun Douala ikiongoza kukata tiketi ya duru ijayo.

Kuna taarifa zisemazo kuwa, hata wachezaji wa kameroun nao walihujumiwa na mashabiki wa Nigeria wa Kwara united.

Stadi wa Bafana Bafana, Beni McCarthy ameendelea kutamba katika Premier League –ligi ya Uingereza:Bao lake la 20 alilotia jana kwa kichwa, liliipa ushindi Blackburn wa mabao 3:1 na kuizamisha Watford mkiani mwa Ligi.

 • Tarehe 19.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcK
 • Tarehe 19.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcK