1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Dunia:Ujerumani yacharuka

Aboubakary Jumaa Liongo14 Juni 2010

Katika mashidano ya kugombea kombe la dunia nchini Afrika Kusini, Ujerumani imeshinda mechi yake ya kwanza kwa kuichabanga Australia mabao manne kwa bila.

https://p.dw.com/p/Nq9W
Waachezaji wa Ujerumani wakishangalia moja ya mabao manne waliyoifunga AustraliaPicha: AP

Washambuliaji, Lukas Podolski na Miroslav Klose waliliona lango la Australia katika dakika  30  za kwanza.

Magoli  mawili ya Ujerumani yaliongezwa  katika kipindi cha pili cha mchezo, na Thomas Müller na Cacau.

Hata hivyo katika kipindi cha pili Australia ilibakiwa na wachezaji 10 baada ya Tim Cahill kuonyeshwa  kadi nyekundu kwa  sababu ya kucheza faulo.

Hapo awali Ghana iliibwaga Serbia kwa  bao moja la penalti  baada mchezaji wa Serbia kuunawa mpira ndani ya eneo nyeti katika dakika ya 86.

Kabla ya mechi hiyo Slovenia  ijipatia ushindi wa kwanza katika mshindano ya kombe la dunia kwa kuifunga Algeria bao moja kwa bila.