Kombe la COSAFA-Castle Cup kuanza | Michezo | DW | 13.02.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kombe la COSAFA-Castle Cup kuanza

Kura imepigwa kwa changamoto za mwaka huu za Kombe la Castle cup.Mabingwa Zambia wanasubiri nuysu-finali.Kaka wa Brazil achukua uraia wa Itali kuongezea ule wa Brazil.

Polisi wazuia fujo katika dimba Leipzig

Polisi wazuia fujo katika dimba Leipzig

Rais wa shirikisho la dimba la Ujerumani –DFB-Theo Zwanziger, ametangaza kwamba mechi zote za kabumbu katika mkoa wa Saxony-mashariki mwa Ujerumani hazitachezwa mwishoni mwa wiki hii. Hii inafuatia mashabiki wahuni kumshambulia polisi jumamosi iliopita mjini Leipzig.Kiasi cha mashabiki 800 wa klabu ya Lokomotive Leipzig waliwahujumu askari 300 kufuatia mpambano wa kuania kikombe cha mkoa huo na kusababisha watu darzeni kadhaa kujeruhiwa .

Na aliekuwa kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani mashariki Georg Buschner, amefariki dunia hapo jana akiwa na umri wa miaka 81.Bushner alikuwa kocha wa Ujerumani mashariki 1970 na anakumbukwa kwa kuipatia taji la olimpik 1976 huko Montreal na hasa alipoingoza GDR-Ujerumani mashariki, kuifunga Ujerumani Magharibi katika Kombe la dunia,1974 nchini Ujerumani .

Taarifa kutoka Itali zasema stadi wa kiungo wa Brazil, Kaka amepata uraia wa Itali miaka 3 tangu kujiunga na klabu ya AC Milan-hii ni kwa muujibu wa La Gazetta dello Sport.

Kaka alinukuliwa kusema,

“Hii ni heshima kuibwa.sasa mimi ni mtaliana na ni Mbrazil.”Hatahivyo, kaka hataweza kuichezea Itali mabingwa wa dunia kwavile alikwisha ichezea Brazil.

Mbrazil mwengine kocha wa Bafana Bafana au Afrika Kusini, Carlos Parreira amepatiwa jana haraka ruhusa ya kufanya kazi na hivyo, amerudi kuwa kocha wa Afrika Kusini.Wizara ya ndani ilikipiga jana faini chama cha mpira cha Afrika Kusini kwa kumfanyisha kazi Parreira -kocha wa zamani wa Brazil bila ruhusa ya kufanya kazi nchini.

Kura imepigwa kwa kinyan’ganyiro cha mwaka huu cha kuania kombe la shirikisho la dimba la kusini mwa Afrika-Castle Cup:

Madagascar ina miadi na Zimbabwe katika Kundi A.Msumbiji itaumana na Seyschelles.Nusu finali itakua April 28.

Katika kundi B, Malawi inakumbana na Afrika Kusini wakati Swaziland ina miadi na Mauritius. Nusu-finali itakua April 26.

Kundi C:Angola inaumana na Lesotho wakati Botswana inacheza na namibia.Washindi wa makundi hayxo 3 wanakutana na mabingwa Zambia katika kura ya nusu-finali ya kombe hilo la COSAFA:

Kura pia imepigwa kwa duru ya pili nay a tatu ya kombe la klabu bingwa za afrika:Young Africans ya Tanzania itakutana na Petro Luanda ya Angola;Desportivo Maputo ya Msumbiji ina miadi na Maelodi Sundwons ya afrika Kusini.Al Hilal ya Sudan itaklutana na majirani zao zamalek ya Misri. TP Mazembe ya J.K.Kongo inakutana na AS Adema ya madagaskar.Mabingwa Al Ahly ya Misri watakumbana na Highlander ya Zimbabwe.

Bajeti ya awali kuandaa kombe la ulaya la mataifa mwakani 2008 nchini Uswisi na Austria, ni Euro milioni 147.Kiasi cha tiketi milioni 1 zitauzwa kuanzia Machi mwakani na finali itachezwa katika Ernst-Happel Stadium Juni 29,2008.

Nje ya dimba, Kenya imeteua leo kikosi chake cha wachezaji 15 kwa kombe la dunia la Cricket huko West Indies.Imekibakisha kikosi kile kile kilichosdhinda taji la dunia mapema mwezi huu.

Maafisa wa michezo kutoka Korea mbili wamekutana leo kujadili kuunda timu ya pamoja kwa michezo ya Olimpik ya mwakani mjini Beijing.

 • Tarehe 13.02.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcg
 • Tarehe 13.02.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcg