1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Afrika:Nani atatamba jioni hii ?

25 Januari 2010

Mabingwa Misri au simba wa nyika Kameroun ?

https://p.dw.com/p/LgSv
Algeria yasonga mbele) nani wa kuizuwia ?Picha: AP

Mabingwa watetezi wa kombe la Afrika, Misri, wana miadi hivi punde na simba wa nyika Kameroun katika kile kinachobainika ni marudio ya finali ya kombe hili mjini Accra-Ghana miaka 2 iliopita.

Na je, mafiraouni wakiwapiga kumbo leo simba wa nyika, tutarajia marudio ya vita vya mahasimu 2 wa kaskazini katika finali ijumapili ijayo:Misri na Algeria ?

Ilikuaje, Tembo wa Ivory Coast,kukanyagwa jana na Algeria ?

Katika bundesliga, Bayer Leverkusen imenyakua usukani kuongoza tena Ligi baada ya Bayern Munich,kuunyakua kwa masaa 24 wakati huko Uingereza, Manchester united nayo imeparamia kileleni mwa Premier League.

Nchini Tanzania, Simba na Yanga zinakamatana koo kuania ubingwa.

Firimbi italia jioni hii (Jumatatu) kuwaita mabingwa wa Afrika ,Misri uwanjani Benguela kwa marudio ya finali ya Kombe lililopita mjini Accra, Ghana na Simba wa nyika, Kameroun. Mpambano huu utakoanza hivi punde utafuatwa na changamoto nyengine ya robo-finali kati ya (super eagles) -Nigeria na Zambia huko Lubango. Kuna uwezekano pia kwamba, finali ya Ijumapili ijayo ya kombe hili ikawa pia marudio ya changamoto ya kufuzu kwa Kombe la dunia Novemba mwaka jana mjini Cairo na Khartoum katika ya mahasimu hawa 2 wa Afrika ya kaskazini -Misri na Algeria.Mpambano uliomwaya damu na kusababisha kuvunjika usuhuba wa kibalozi.

Bundesliga na Premier League:

Bayer Leverküsen ,imeunyakua tena usukani ili kuongopza Bundesliga-ligi ya Ujerumani jana baada ya kuibomoa Hoffenheim, kwa mabao 3-0.Alikuwa tena jogoo lao waliloliazima kutoka Bayern Munich,Toni Kroos,lililowika kwa bao maridadi na kuandaa 2 mengine.Leverkusen, ikiongozwa na kocha Jupp Heynckes,mwishoe, imeondoka na pointi 3 baada ya kutoka sare mara 5 zilizopita.Ilianza pole pole ,lakini kilipoingia kipindi cha pili,Leverkusen ilishika usukani wa mchezo kama kocha mwenyewe Heynckes anavyosimulia:

"Kipindi cha kwanza ,hatukuweza kudhibiti mchezo na wala hatukutamba, lakini, tulipobadili mchezo kipindi cha pili na kuongoza kwa mabao 2:0, tulianza kutamba na tukaibuka timu bora kipindi cha pili."

Mabingwa Wolfsburg, walicjhezeshwa jana kindumbwe-ndumbwe tena nyumbani mwao na kuaibishwa na FC Cologne, iliowakandika mabao 3:2 na kuzidisha misukosuko ya kocha Armin Weh.

Mabao ya Kevin Pezzoni,Sebastian Freis na Adil Cihi,yalitosha kuzidisha misukosuko ya mabingwa.Mabingwa Wolfsburg ,walirudi lakini kusawazisha hadi mabao 2:2 ,lakini mwishoe, mmorocco Cihi, aliupiga msumari wa 3 katika jeneza la mabingwa na kuipa Cologne ushindi usiotarajiwa kabisa.

Cologne ilitamba mbele ya mabingwaWolfburg,licha ya kucheza bila ya mastadi wake 2 maarufu-mshambulizi Lukas Podolski na mwenzake Milivoje Navokovic .

Sasa Cologne imejikomboa kutoka orodha za timu 3 zinazoweza kuteremshwa ikiwa imeangukia nafasi ya 13 ya ngazi ya Ligi. Sasa, hatima ya kocha wa Wolfsburg, Armin Weh, iko mashakani. Bayern Munich, ilizima vishindo vya Werder Bremen, Jumamosi na mwishoe, kuwakandika mabao 3-2 na kutoroka na pointi 3. Schalke ilimudu suluhu tu ya mabao 2:2 na Bochum ,baada ya kutangulia kwa kishindo.

Amakatika Premier League,Manchester United, imetumia fursa ya mahasimu wao Chelsea, kushughulika na kombe la FA na kuparamia wao kileleni mwa Premier League kwa mara ya klwanza tangu Oktoba.Manu, imeitandika Hull City mabao 4-0.Ilikua Wayne Rooney, alielifumania lango la Hull City kwa mabao hayo yote.

Mwandishi: Ramadhan Ali / APE/DPAE/RTRE

Uhariri: Othman Miraji