Kitisho cha itikadi kali ya dini ya kiislam kuingia Senegal | Matukio ya Afrika | DW | 21.02.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Kitisho cha itikadi kali ya dini ya kiislam kuingia Senegal

Wadadisi wameingiwa na wasi wasi wanamgambo wa Al Qaida katika eneo la Maghreb.Aqmi wasije wakaitumia hali ya mambo na kujipenyeza Senegal.

default

Rais Abdoulaye Wade wa Senegal

Uchaguzi wa rais umepangwa kufanyika nchini Senegal februari 26 ijayo.Hadi wakati huu nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilikuwa ikiangaliwa kama mfano mzuri wa kufuatwa katika eneo hilo ambalo ni tete.Kinyume na nchi jirani za Mali na Mauritania,Senegal haijazongwa na visa vya magaidi wa Al Qaida katika eneo la Maghreb-Aqmi.Lakini hali hiyo inaweza kubadilika,na Aqmi kueneza ushawishi wake pia nchini Senegal.Mfano rais Abdoulaye Wade,licha ya maandamano ya umma,atakapopigania mhula wa tatu na Senegal kutumbukia katika janga la vurugu za kisiasa.

Tayari mnamo mwaka 2010 Senegal iliwafukuza wamauritania waliokuwa wakituhumiwa kuwa wafuasi wa kundi la magaidi wa Al Qaida katika eneo la maghreb-Aqmi.Mwaka 2011 mjumbe maalum wa zamani wa umoja wa mataifa kwa eneo la Afrika magharibi,Ahmed Ould Abdallah wa kutoka Mauritania alionya dhidi ya kuwepo wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam nchini Senegal.Mwezi january Umoja wa Mataifa ukatuma ujumbe katika eneo la Sahel:lengo lilikuwa kukusanya maelezo kuhusu hatari ya kuvurugika utulivu na usalama wa eneo hilo baada ya kuporomoka kiongozi wa Libya Muammar al-Gaddafi.

Mahabusi waliowahi kutekwa nyara na wanamgambo wa Aqmi walisema walinzi wao walikuwa wasenegal.

Muandishi habari wa Senegal Mame Less Camara,mdadisi wa miaka mingi wa masuala ya kisiasa na kidini anahisi kuna vyenzo vingi tu vinavyoweza kurahisisha kujipenyeza wanamgambo wa Aqmi nchini Senegal:Anaonya kwa kusema"Nchini Senegal dini ina nguvu zaidi kuliko siasa.Ndio maana tunaweza kuona picha kwa mfano jinsi rais Wade anavyompigia magoti khalifa mkuu.Ingawa huku hatuna mfumo wa kidini,lakini tuna utaratibu ambao wawakilishi wa dini ndio wanaotoa muongozo kuhusu mipaka ya uvumilivu."

Senegal Proteste Regierung

Vikosi vya usalama vyapambana na waandamanaji

Senegal pia imeimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi pamoja na Saud Arabia,nchi alikotokea kiongozi wa zamani wa magaidi Ben Laden ,nchi kunakokutikana makundi tofauti ya nadharia kali ya dini ya kiislam.

Maimam wa Senegal wanapatiwa mafunzo yao katika zile nchi ambako vyuo vya kiislam vinafuata itikadi kali:nchini Misri,Mataifa ya Ghuba na Libya.Mawasiliano na Nigeria au pengine pia na kundi la magaidi la Boko Haram? Hayo yapo tangu zamani.Kwasababu muridi nchini Senegal wanawaandikisha zaidi waumini kutoka nchi jirani ya Nigeria.Na kadhia hiyo hasa ndiyo inayomtia wasi wasi mkubwa zaidi Mame Less Camara kuhusu vijana nchini mwake ambao mara nyingi wanajikuta hawana kazi na hawana mustakbal wowote.

Kitisho cha kuibuka itikadi kali ya dini ya kiislam na mshikamano pamoja na kundi la magaidi wa Maghreb- Aqmi kinakutikana zaidi katika zile nchi ambazo ni dhaifu.Nchini Mali na Mauritania-majirani wa karibu zaidi na Senegal,wanamgambo wa Aqmi wameshaingia.Nchini Niger pia wana nguvu na mawasiliano yapo pia pamoja na Boko Haram wa Nigeria.Ugonvi kuhusu azma ya rais Abdoulaye Wade kutaka kugombea mhula wa tatu baada ya kuifanyia marekebisho katiba unazusha hofu Aqmi wasije wakajipenyeza pia nchini Senegal.

Senegal Proteste Regierung

Maandamano dhidi ya serikali mjini Dakar

Wataalam wa masuala ya ugaidi mfano wa mfaransa Jean-Charles Brisard anatuliza hofu hizo akisema Senegal iko mbali sana na kuangukia mikononi mwa Aqmi.

Hata Abdoul-Aziz Kébé ,mtaalam wa masuala ya dini ya kiislam katika chuo kikuu cha Cheikh Anza Diop mjini Dakar haoni kama kuna hatari yoyote kwa sasa.Kwa maoni yake muridi nchini Senegal ni kinga dhidi ya itikadi kali ya dini ya kiislam.

Mwandishi:Köpp,Dirke (MM Regionen Afrika/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul-Rahman Mohammed