KISMAYU: Maelfu ya wasomali waukimbia uwanja wa vita | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KISMAYU: Maelfu ya wasomali waukimbia uwanja wa vita

Maelfu ya wasomali wameanza kuukimbia uwanja wa vita huku wanajeshi wa Ethiopia waliojihami na silaha nzito wakisaidiwa na ndege za kivita wakiikaribia ngome iliyosalia ya wanamgambo wa mahakama za kiislamu mjini Kismayu.

Wasomali takriban 2,000 wamebeba walichoweza na kuukimbia mji wa kusini wa Jilib ambako wanamgambo wasiopungua 3,000 wa mahakama za kiislamu wamejificha kati ya mpaka wa Kenya na bahari ya Hindi wakijiandaa kupigana kufa kupona na majeshi ya Ethiopia.

Mabomu ya kutegwa ardhini yaliyozikwa kwenye njia inayoelekea Kismayu yanawachelewesha wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia na majeshi ya Ethiopia kuufikia mji huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com