1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KISMAYO: Hofu ya kuzuka mapigano mapya Somalia

Kundi la wanamgambo lililodhibiti bandari ya Kismayo hadi mji huo kutekwa na Muungano wa Mahakama za Waislamu mwezi uliopita,limekula kiapo kuwa litaudhibiti tena mji huo.Tangu kuuteka mji mkuu wa Mogadishu mwezi wa Juni, Muungano wa Waislamu umezidi kudhibiti sehemu zingine za Somalia na kuiacha serikali ya mpito bila ya usemi mkubwa.Muungano huo lakini umekabiliwa na maandamano makali ya upinzani baada ya kuuteka mji wa Kismayo ulio wa tatu kwa ukubwa nchini Somalia.Siku ya Ijumaa waandamanaji 100 walikamatwa baada ya vikosi vya Muungano kufyatua risasi hewani kuyavunja maandamano.Siku hizi chache za nyuma,zaidi ya Wasomali 2,000 wamekimbilia Kenya wakiwa na hofu kuwa mapigano mapya yatazuka katika eneo la Kismayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com