1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kipchoge, Kipsang kukutana London marathon

Bingwa mtetezi wa mbio za London Marathon Eliud Kipchoge wa Kenya atapambana na mshindi wa mwaka wa 2014 wa mbio hizo mwenzake Wilson Kipsang katika mashindano ya mwaka huu

Waandalizi wamesema wanariadha hao wote wamethibitisha kushiriki katika kivumbi hicho cha Aprili 24.

Kipchoge, ambaye kwa sasa anaongoza katika msimamo wa viwango vya kimataifa, alimpiku Kipsang, mwenye umri wa miaka 33, katika mashindano ya mwaka jana ya London marathon, kwa sekunde tano tu na pia akashinda mbio za Berlin Marathon mwaka wa 2015, ambako aliweka muda wake bora wa saa mbili dakika nne.

Ghirmay Ghebreslassie, ambaye aliibuka kuwa bingwa wa marathon mwenye umri mdogo zaidi ulimwenguni mjini Beijing mwaka jana, pia ametangaza kuwa atashiriki kwa mara ya kwanza katika London marathon.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Mohamed Khelef